KIJANA Carl Griffiths, 19, (pichani) ndiye mwanaume mwenye miguu mirefu duniani. Kituko ni kwamba anatumia ukubwa wa miguu yake kunasa wanawake.
Carl, raia wa Uingereza, amesema kuwa mpaka sasa ameshatoka kimapenzi na wanawake 30 ambao walidata kwake kutokana na urefu wa miguu yake.
Amesema kuwa wanawake wengi wanavutiwa naye kwa kuamini kwamba ana kitu cha ziada kwenye mapenzi kutokana na ukubwa wa miguu yake.
Pamoja na umri mdogo alionao, miguu ya Carl ina ukubwa wa ‘saizi’ namba 21, ikiwa ni mara mbili zaidi ya kipimo cha miguu ya wanaume wa kawaida nchini Uingereza.
Kwa kawaida, Waingereza miguu yao ni namba tisa na wale wenye mikubwa, hufikia namba 10, kwa hiyo umbile la miguu ya Carl ni ajabu kutokea.
Kutokana na hali hiyo, Carl hutoa oda maalum kwa ajili ya kutengenezewa viatu vyake.
Carl, ambaye anaishi Trimsaram, kusini ya Wales, Uingereza, amekuwa akichati kwenye mitandao ya kijamii inayozungumzia wanaume wenye miguu mikubwa na kutoa siri zake mbalimbali.
Akitoa siri zake, Carl alisema: “Wanawake wamekuwa wakinitaka mimi kwa kitu kimoja tu, kwa hiyo hawanisumbui.
Carl alisema, miguu yake ni mikubwa mno na hakumbuki ilianza kukua lini.
“Ilikua kwa haraka mno, nilipokuwa shule mama alikuwa anahangaika kuninunulia viatu vipya kila mwezi . Kila mwaka nilikuwa nanunuliwa pea mbili au tatu.
“Nilipokuwa na umri wa miaka 12, nilikuwa navaa namba 14 ya viatu. Miaka miwili baadaye, nilikuwa navaa namba 17. Nilikuwa nacheza mpira na nimehangaika sana kutafuta buti la kuchezea soka mpaka nilipotengenezesha oda maalum kutoka Marekani.”
“Kila kiatu huwa nalipia pauni 100 (shilingi 270,000), pauni 50 ninapotoa oda na pauni 50 hulipa ninapoanza kuvaa.
“Kwa sasa nina jozi moja ya mazoezi na nyingine kwa ajili ya kazi. Mara nyingi nikiingia klabu, watu huacha mambo yao na kuniangalia. Watu wanaopita jirani yangu, hunikanyaga lakini huwa sijali.”
Baba wa Carl, Griffiths mwenye umri wa miaka 39, alisema: “Sijui mwanangu amepata wapi hii miguu kwa sababu hajanifuata mimi wala mama yake.”
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment