Stori: Jelard Lucas
KANISA la Romani Katoliki limeishukia tasnia ya filamu Bongo (Bongo Movies) kutokana na matendo maovu yanayofanywa na wasanii katika sinema zao hususan suala zima la kuheshimu imani za watu.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi.
Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo hawakubaliani nayo.
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.
CHANZO: GPL
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment