Kwanza kabisa pole na majukum yako ya kila siku ya kujenga mahusiano yaliyo bora yenye amani na Upendo wa dhati, usiyo kwisha hamu.

Najua wazi kuwa siyo wote, wanafurahia blog hii ila wengi wanaipenda kwa kuwa wanajifunza mambo mengi kila wakati wanapoingia humu ndani.

Kuna wale waliyoathiriwa kimapenzi kwa hiyo, awana muda wa kujua kinachoendelea katika ulimwengi wa mapenzi, wengine basi hawajali, wenyewe wanajifanya wanajua kila kiti.

Pamoja na yote kuna kundi kubwa la wanaume wanaoshindwa kueleza hisia zao moja kwa moja kwa wale wanaovutiwa nao na kutamani pengine kuwa nao maishani.

Hii inawaumiza vijana wengi na hata wazee, suala la kutengeneza sentensi mpaka aweze kumweleza mwanamke amuelewe, inamchukua muda sasa wanatumia marafiki amabo wengi huwageuka.

Hatua hii husababisha baadhi kujiona wenye mkosi wa kupendwa na warembo jambo ambalo siyo la kweli.

Sifa ya kwanza ili uweze kuzungumza na mwanamke akusikilize ni lazima ujiamini, kuwa wewe ni mwanaume mwenye vigenzo vya kuitwa mwanaume, unayeweza kusiamama mbele ya wanaume wengine wakasema mimi ndiye mmiliki wa mwanamke huyu.

Pili wanawake wanapenda kuwa katika ushindani hasa pale anapokuwa na mwanaume mwenyekujiamini basi anatembea akijiamini na kuona hajakosea kuchagua.

Kwanini wewe hujui kutongoza, siyo kwamba hujui tatizo hujiamini tu ndiyo maana inakuwa ngumu kuunga mistari yako na kumweleza mwanamke akakuelewa.

Neno nakupenda lina herufi 9 ila ni gumu sana kutamkwa na wengi, na unaweza ukamwambia mwanamke nakupenda akakuhoji kama askari polisi wewe usiogope endelea kumweleza unachompendea bila kusitasita wala kung’ata maneno.

Kwa kufanya hivyo utafaulu mtihani wako vizuri na mwanamke aliye makini atajua amepata mwanaume ambaye anajiamini.

Acha kuogopa huu ni wakati wako wa kuendelea kutembelea mahabati ili kuelimika zaidi katika anga ya mahusiano ya kimapenzi.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment