Msanii aliyepata kuvuma sana kabla ya mwaka 2010 alimaarufu kwa jina la Marlaw, amejutia uamuzi wake wa kukipigia kampeni chama cha ccm kwani kimemporomosha kimuziki.


"Unajua mimi mwaka 2010 nimeburudisha ktk kampeni za ccm lakini nimeambulia kushuka kimuziki sijui ni siasa imehusika au la kwa sababu toka hapo nimetoa nyimbo nyingi lakini hazivumi tena, sasa sitaipigia ccm tena labda chama kingine si unajua vijana wako wapi mzee ha ha haaa si kwamba nimejitoa ccm hapana mi ni msanii naburudisha watu wote" 


Mwananchi lilipotaka kujua ni chama gani amekilenga kukipigia kampeni kwa malipo alisema bado muda wa kukiweka hadharani.


Wasanii someni alama za nyakati msije jikuta mko njia panda kimuziki huu ni mfumo wa vyama vyama vingi.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment