UMOJA wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo huo mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa
habari, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe
amesema wabunge wote kutoka katika vyama vinavyounda umoja huo
hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao kuwa hawajaadhibiwa.
Umoja huo pia umemtaka Rais Kikwete kutotia saini miswada hiyo kwa kuwa imepitishwa kinyume na taratibu.
Mbowe amesema kuwa endapo Rais Kikwete atalazimisha kuisaini miswada hiyo, umoja huo utaishitaki serikali kwa wananchi.
Wabunge wote kutoka UKAWA wameazimia kuondoka kabisa leo kutoka mjini
Dodoma, na wanataraji kukutana jijini Dar es salaam siku ya Jumatano
kwa hatua zaidi.
Wakati huo huo bunge limepitisha muswada wa usimamizi wa mapato
yatokanayo na mafuta na gesi, na muswada mwingine wa uwazi na
uwajibikaji katika uchimbaji wa madini, gesi na mafuta, hiyo ikiwa ni
miswada miwli kati ya mitatu ambayo imekuwa ikipingwa na wabunge kutoka
UKAWA.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment