Kamati ya Lembeli ambayo leo imesoma Taarifa ya Uchunguzi ya Kamati kwa Bunge imependekeza Waziri wa Maendeleo na Uvuvi, Dk David Mathayo David , Mkurugezi wa Wanyamapori na maofisa wengine wajiuzulu mara moja kutokana na kuwapo kwa matukio ya kuchomwa moto kwa nyumba za wananchi na kuuawa kwa baadhi ya watu wakati wa operesheni tokomeza majangili.
Bunge Limeharishwa kwa muda ili kujadili muda uliopendekezwa na Wabunge wa kujadili ripoti ya uchunguzi ya Lembeli kuhusu mauaji na nyumba kuchomwa moto wakati operesheni tokomeza majangili nchini.
Katika taarifa hiyo, imependekezwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David ajiuzulu, mkurugenzi wa Wanyamapori Tanzania, maofisa wa jeshi na mgambo waliohusika katika mauaji hayo wawajibishwe.
<<Habari Mpya >.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment