Ukianza kutaja nyimbo zilizofanya vizuri mwaka 2012 basi lazima utaje wimbo unaofahamika kwa jina la 'Nidanganye Nidanganye' uliyoimbwa na Shetta aliyomshirikisha Naseeb Abdul aka Diamond Platium
Sasa habari njema nyingine kutoka kwa Shetta akizungumza na tovuti ya 100.5 leo Novemba 28 amesema kwasasa yupo katika hatua ya maandalizi ya wimbo wake mpya 'Mama Qayllah' aliyomshirikisha Diamond Platinum,wimbo umetengeneza Burn Records chini ya producer 'Sheddy Clever'
'Shetta hapa ama niite Baba Qayllah,kwanza kabla ya yote ningependa kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea vizuri video ya wimbo wangu 'Sina Imani',kwa sasa nipo katika maandalizi ya wimbo wangu mwingine mpya kabisa humo ndani nipo mimi pamoja na Diamond,wimbo unaitwa Mama Qayllah bado upo katika hatua za mwisho za kufanyiwa mixing na Sheddy Clever wa Burn Records,Kwa hiyo wewe shabiki kaa tayari hapa Baba Qayllah pale Platinum ebu Angalia Mbele'Alisema Shetta.
Katika mazungumzo Shetta alidai kuwa huu ndio utakuwa ni wimbo wake wa kufungia Mwaka 2013
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment